Simu feki zazimwa Tanzania

Jun 17, 2016, 05:48 PM

Zaidi ya watu laki sita nchini Tanzania hawana mawasiliano ya Simu baada ya Simu zao ambazo hazina ubora kuzimwa na mamlaka ya mawasiliano nchini humo.

Hata hivyo kumekuwa na maoni tofauti kufuatia baadhi ya wanaomiliki simu ambazo hazina viwango kuendelea kupata mawasiliano huku mamlaka ya mawasiliano kusema kuwa Simu hizo zitaendelea kuzimwa.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda ametutumia taarifa ifuatayo.

#simu #feki #bandia #Tanzania #TCRA